IQNA

Harakati za Kiislamu Palestina

Msimamo wa Saudia mbele ya Munafikina ni kwa Maslahi ya Israel

16:40 - July 11, 2016
1
Habari ID: 3470447
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas, na Harakati ya Palestina ya Jihad Islami zimelaani matamshi ya mwanamfalme wa Saudia katika kikao cha munafikina huko Paris.

Katika taarifa, Hamas na Jihad Islami zimesema matamshi ya mwanamfalme Turki al Faisal katika kikao hicho cha kundi la kigaidi la munafikina maarufu kama MKO siku ya Jumamosi mjini Paris ni kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Akizungumza katika kikao hicho cha munafikiana wanaopinga mfumo wa Kiislamu Iran, Faisal ambaye aliwahi kuwa mkuu wa shirika la kijasusi la Saudia, alidai kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaunga mkono Hamas na Jihad Islami huko Palestina kwa lengo la kuibua machafuko katika eneo.

Katika taarifa, Jihad Islami imesema: "Tunawaambia kuwa, iwapo hamuungi mkono Palestina, kwa uchache basi msiunge mkono utawala wa Kizayuni." Jihadi Islami imesema wananchi Waislamu Saudia hawatakubali nchi yao ifungue njia ya Waisraeli kufika Makka na Madina.

Kwa upande wake, Hamas ililaani matamshi ya Faisal na kuyataka kuwa yasiyo na msingi. "Kila mtu anafahamu kuwa Hamas ni harakati ya Palestina inayopigana dhidi ya Wazayuni wanaokalia kwa mabavu ardhi ya Palestina na inafuatilia kadhia ya Palestina pekee." Hamas imesema Faisal anatumikia maslahi ya Wazayuni maghasibu na kuchochea hujuma dhidi ya watu wa Palestina.

Kikao cha kundi la kigaidi la Munafikina huko Paris, Ufaransa na matamshi yaliyotolewa na Turki Faisal Mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Saudi Arabia mbele ya wanachama wa kundi hilo kwa mara nyingine tena yameonyesha namna Saudia inavyoendelea kutumia ugaidi kama stratejia ya kufanikisha malengo ya utawala wa Aal Saud katika eneo.

Turki al Faisal Mwanamfalme wa Saudi Arabia katika kikao hicho cha munafikina,  aliliahidi ushindi kundi hilo la kigaidi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kudai kuwa Iran inaingilia masuala ya ndani ya nchi za Kiarabu na kwamba Riyadh itazuia uingiliaji huo. Turki al Faisal aliyasema hayo katika mkutano wa kila mwaka wa kundi la kigaidi la Munafikina, kundi ambalo kwa miaka kadhaa sasa linatekeleza vitendo vya kigaidi kwa kuungwa mkono na nchi za Magharibi.

Matamshi ya juzi ya Turki al Faisal bila shaka ni aina fulani ya sisitizo la kushikamana na kuendeleza mashirikiano ya karibu kati ya magaidi hao wenye faili jeusi na utawala wa Saudia

Katika kipindi cha miaka karibu 40 sasa,  kundi la kigaidi la munafikina limetekeleza jinai na kuwaua shahidi raia na maafisa wa ngazi za juu Iran takribani 17000, jinai ambazo hazitasahaulika katika fikra za jamii ya wanadamu na daima magaidi wa kundi hilo watachukiwa na kustahiki adhabu kali.

3514066

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Bila jina
0
0
Laana za mwenyezi mungu ziwafike serikali ya K.S.A,wameuza uislamu kwa macowboy na na wazayuni ilhali wanajua uislamu ndiyo utabaki na ushindi
Takbirr Allah akbar
captcha