IQNA

Katika kikao cha Malaysia

Wanasayansi Waislamu watakiwa kusuluhisha matatizo

14:59 - December 24, 2016
Habari ID: 3470756
IQNA: Mkutano wa kwanza wa Mabadilishano ya Sayansi na Teknolojia miongoni mwa nchi za Kiislamu (STEP) umefanyika katika mji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kikao hicho kimeandaliwa kwa pamoja na Taasisi ya Sayansi na Teknoloaji ya Mustafa SAW na Chuo Kikuu cha Malaysia.

"Tuko hapa kusuluhisha matatizo yetu na wala si kulalamika kuhusu matatizo hayo," alisema Omar Yaghi mwanakemia kutoka Jordan wakati akihutubia wajumbe waliohudhuria kikao hicho.

Watafiti 150 kutoka nchi 30 Misri, Morocco, Oman, Jordan, Saudi Arabia, Iran, Pakistan, India, Bangladesh, Malaysia, Singapore na Uturuki wameshiriki kikao hicho.

Taasisi ya Sayansi na Teknoloaji ya Mustafa SAW imesema kikao hicho kitakuwa kikifanyika mara kwa mara pengine mara moja kwa miaka miwili au mara moja kwa mwaka.

Moja ya malengo ya kikao hicho ni kuwaenzi wanasayanis Waislamu kwa kuwatunuku zawadi ijulikanayo kama Zawadi ya Mustafa SAW.

Mkutano huo ulianza Disemba 19 hadi 22 ambapo katika siku ya mwisho kulifanyika sherehe maalumu.

3461746

captcha