IQNA

Kongamano la Kimataifa la Qur'ani, Hadithi kufanyika Indonesia

13:44 - December 26, 2016
Habari ID: 3470762
IQNA: Kongamano la Pili la Kimataifa la "Elimu ya Kiislamu na Utafiti wa Qur'ani na Hadithi za Mtume SAW" limepangwa kufanyika mjini Mataram, Indonesia Machi 2017.
Kongamano la Kimataifa la Qur'ani, Hadithi kufanyika Indonesia

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo limeandaliwa na Jarida la Utafiti wa Kiislamu la Ulumuna, ambalo huchapishwa mara moja kila miaka miwili katika Taasisi ya Kitaifa ya Kiislamu Indonesia mjini Mataram.

Kwa mujibu wa jarida la Ulumuna, kongamano hilo litafanyika Machi 11, 2017 ambapo mada kuu itakuwa "Elimu ya Kiislamu na Utafiti wa Qur'ani na Hadithi".

Jarida hilo limesema linapokea Makala ambazo zimeandikwa kwa mujibu wa utafiti wa maktaba au katika medani na kwamba Makala zinaweza kuhusu maudhui za siasa, anthropolojia, ethnografia, na masomo ya kidini.

Aidha watafiti wanaweza kuandika Makala kuhusu shule za kidini (madrassah) na za academia, ufundishaji sayansi na dini katika chule za Kiislamu, ufundishaji Uislamu katika shule zenye watu wa dini na tamaduni mbali mbali, na malezo bora.

Halikadhalika watafiti wanaweza kuandika Makala kuhusu Qur'ani na Hadithi na mtazamo wa wasomi Waislamu na Wamagharibi kuhusu Qur'ani na Hadithi. Siku ya mwisho ya kuwasilisha makala imetajwa kuwa Januari 31 2017. Kwa maelezo zaidi kuhusu kongamano hilo bonyeza hapa.


3556636



captcha