Rais Hassan Rouhani ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya kitaifa ya mwaka 38 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Medani ya Azadi mjini Tehran. Amesisitiza kuwa, mapinduzi hayo yalikuwa tukio muhimu katika historia ya Iran kwa kuikomboa nchi kutoka kwenye utegemezi wa wageni hususan Marekani na kuwawezesha wananchi kushika hatamu za nchi yao.
Dakta Rouhani amesema kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni
mapinduzi ya kwanza duniani ambao chini ya miezi miwili tu baada ya
kutokea kwake wananchi wake walikwenda kwenye masanduku ya kupigia kura
na kuchagua mfumo wa utawala wanaoutaka wao wenyewe.
Rais Rouhani amesema kuwa,wanagenzi walioshika madarakani katika baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati na huko Marekani wanapaswa kuelewa kwamba, wanalazimika kuzungumza na taifa la Iran kwa heshima na taadhima. Amesema jibu la taifa la Iran kwa vitisho vya adui litakuwa kali na kuongeza kuwa, wale wanaoitishia serikali na jeshi la Iran wanapaswa kuelewa kuwa, wananchi wa Iran watajitokeza kukabiliana nao kwa nguvu, umakini na mantiki katika mpambano muhimu zaidi wa historia.
Rais wa Iran amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu kamwe haitaki kuzusha mivutano lakini wale wanaolitakia mabaya taifa la Iran wanapaswa kujiepusha na uchokozi wa aina yoyote dhidi ya taifa hili.
Kuhusu maendeleo ya Iran katika medani ya nyuklia na mafanikio ya wasomi
hapa nchini ya kutengeneza mashinipewa aina ya IR-8, Rais Rouhani
amesema kuwa, hadi kufikia mwaka jana maadui wa maendeleo na ustawi wa
Iran hawakuruhusu kuingizwa nchini hata gramu moja ya keki ya njano
lakini hivi majuzi tu zimeingizwa nchini tani 350 za unari na keki ya
njano.
3572796/