IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Sala ya Idul Fitr

Migogoro Yemen, Kashmir na Bahrain ni jeraha kubwa katika umma wa Kiislamu

15:15 - June 26, 2017
Habari ID: 3471037
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, migogoro ya Yemen, Kashmir na Bahrain ni jeraha kubwa linaoukabili umma wa Kiislamu.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo leo asubuhi mjini Tehran katika hotuba ya swala ya Idul Fitr iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran ambapo ameutaka umma wa Kiislamu kusimama imara na kuisaidia Yemen kwa namna ya wazi kabisa kutokana na ukatili inaofanyiwa. Amesisitiza kwa kusema: "Ni lazima maulamaa wa Kiislamu wachukue hatua kuhusiana na kinachojiri katika baadhi ya nchi za Kiislamu hata kama suala hilo litawakasirisha makafiri." Kiongozi Muadhamu ametahadharisha kuwa migogoro inaibuliwa katika ulimwengu wa Kiislamu ili kuwasahaulisha Waislamu kadhia ya Palestina ambayo ni muhimu zaidi katika umma wa Kiislamu.

Kadhalika amezungumzia mafanikio mbalimbali ya kimaanawi yaliyopatikana ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani uliomalizika jana Jumapili, yakiwemo matendo ya ibada na kusema kuwa, shambulio la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGCdhidi ya magaidi katika mji wa Deir Ezzor nchini Syria, ni amali tukufu ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kushiriki kwa wingi watu katika matembezi ya siku hiyo tukufu ni miongoni mwa matukio muhimu yaliyotokea ndani ya mwezi humo mtukufu wa Ramadhani. Swala ya Idul Fitr nchini Iran imeswalishwa kitaifa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei hapa Tehran, ambapo idadi kubwa ya Waislamu wa mji wa Tehran wameshiriki swala hiyo. Halikadhalika mabalozi wa nchi za Kiislamu Tehran wameshiriki katika sala hiyo.

Baraza la Idul Fitr Tehran

Wakati huo huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa, kwa mujibu wa fiqhi ya Kiislamu, Waislamu wote wanawajibika kupambana na kupigana jihadi kwa kutumia njia zote zinazowezekana dhidi ya adui anayevamia na kukalia kwa mabavu ardhi ya Kiislamu; kwa msingi huo hii leo ni wajibu kwa ulimwengu mzima wa Kiislamu kupambana na utawala ghasibu wa Israel.

Ayatullah Khamenei aliyasema hayo leo alipohutubia Baraza la Idil Fitri lililowakutanisha pamoja viongozi, matabaka mbalimbali ya wananchi na mabalozi wa nchi za Kiislamu mjini Tehran nakutoa mkono wa Idi kwa Waislamu wote. Amekosoa hatua ya baadhi ya nchi za Waislamu ya kukataa kushiriki katika mapambano hayo ya jihadi na kusema kuwa, taifa la Iran liko makini na pevu katika kutekeleza wajibu na majukumu yake. Ameongeza kuwa: Ulimwengu wa Kiislamu unahitajia kuwa na umoja na mshikamano na kwamba aghlabu ya mataifa ya Waislamu yako pamoja na yanashikamana na kuwa, ni wajibu wa serikali za nchi za Waislamu pia kutekeleza majumu yao.

Amesisitiza kuwa,kupuuza na kulisahaulisha suala la Palestina ni hatari kubwana kuongeza kuwa: Umoja na kujiepusha na mifarakano vina maslahi kwa nchi za Kiislamu na kwamba, kuna udharura wa kuzuia mipango ya kuufanya Umma upuuze na kusahau kadhia ya Palestina ambayo ni kadhia nambari moja ya Umma wa Kiislamu, kwa kushirikiana zaidi katika suala hilo.



3463219
captcha