IQNA

13:59 - May 18, 2019
News ID: 3471962
TEHRAN (IQNA)- Mwanamke mmoja Mjapani anasema mashambulizi ya Septemba 11 2001 nchini Marekani yalimpelekea afanye utafiti wa kina kuhusu Uislamu na hatimaye akaamua kusilimu.

Akizungumza Ijumaa katika hafla malumu ya 'Walioweza Kupata Njia ya Haki' katika Maonyesho ya 27 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran, Bi. Fatimah (Atsuku) Hushino anasema baada ya matukio ya 9/11, vyombo vya habari vilianza propanda kali dhidi ya Uislamu.

Anasema hiyo ilikuwa cheche ya kumfanya atake kuujua zaidi Uislamu badala ya kutegemea propaganda za vyombo vya habari.

"Baada ya utafiti wwa kina, niliweza kufahamu bayana kuwa vyombo vya habari vinaenza hadaa na urongo kuhusu Uislamu. Kuptia ami yangu, ambaye alikuwa amebadili dini na kuwa Mkristo, nilikuwa naifahamu Bibilia kwa kiasi fulani na hapo nililinganisha na Qur'ani Tukufu na hatimaye nikafikia natija kuwa Kitabu Kitukufu cha Uislamu kimekamilika."

Akijibu swali kuhusu mtazamo wa familia yake baada ya kufahamu kuwa ameukumbatia Uislamu, Bi. Hushino anasema walipinga vikali uamuzi wake huo na hata walijaribu kumshawishi awe Mbuddha.

"Walipinga sana uamuzi wangu huo hasa vazi langu la Hijabu," ameongeza na kusema kuwa, hatimaye walikubali ukweli kuwa ameuchagua Uislamu maishani.

Maonyesho ya 27 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran yanafanyika katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini huku nara kuu mwaka huu ikiwa ni "Qur'ani Maana ya Maisha". Maonyesho hayo yanatazamiwa kuendelea hadi Mei 24.

Kila siku katika kitengo cha kimataifa cha maonyesho hayo, waliosilimu huweza kusimulia kile kilichowapelekea kuuchagua Uislamu maishani.

3812491

Name:
Email:
* Comment: