IQNA

Maonyesho ya Qur'ani

Kauli mbiu ya Maonyesho ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani yatangazwa

17:21 - March 04, 2024
Habari ID: 3478448
IQNA – Awamu ya 31 ya Maonesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Tehran imepangwa kuzinduliwa baadaye mwaka huu na sasa waandaaji wamechagua kauli mbiu ya tukio hilo.

Kama maonyesho yaliyopita, maonyesho ya mwaka huu yatafanyika yenye kauli mbiu ya "Ninakusoma".

Ukumbi wa Salah (Mosallah) wa Imam Khomeini (RA) utakuwa mwenyeji wa hafla hiyo ya kimataifa ya Qur'ani kuanzia Machi 21 hadi Aprili 3.

Kufikia sasa, nchi 25 zimetangaza utayari wao wa kushiriki katika sehemu ya kimataifa ya maonyesho hayo.

Mwaka huu, suala la Palestina na mapambano ya watu wa Palestina- hususan Ukanda wa Gaza, Lebanon na Yemen ndio mada kuu za sehemu ya kimataifa.

Maonesho ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran kila mwaka huandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maonyesho hayo yanalenga kukuza ufahamu wa Qur'ani na kuendeleza shughuli za Qur'ani nchini Iran na katika uga wa kimataifa..

Aidha maonyesho hayo huwa kituo cha kuwasilisha mafanikio ya hivi punde zaidi ya Qur'ani nchini Iran na pia huuzwa bidhaa mbalimbali zinazohusiana na Qur'ani.

4203233

Habari zinazohusiana
Kishikizo: maonyesho ya qurani
captcha