IQNA

Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajioun
12:31 - September 05, 2019
News ID: 3472116
TEHRAN (IQNA) – Mwanamke wa Russia aliyesilimu na kisha kutarjumi Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kirussia amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Russia, Bi. Valeria Porokhova alifariki Jumtatu. Tarjuma yake ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kirussia imetajwa kuwa miongoni mwa bora zaidi.

Porokhova alizaliwa Tsarskoye Selo, Russia na alikuwa Mkrito wa Othodoxi kabla ya kusilimu baada ya kuolewa na mwanazuoni wa Kiislamu kutoka Syria. Alihamia katika mji mkuu wa Syria, Damascus mwaka 1985.

Baada ya kujifunza Kiarabu, alianza kuandika tarjumi ya Qur'ani kwa lugha ya Kirussia  na kazi yake imetajwa kuwa ya kipekee kwa ubora wa fasihi na ufahamu ilikiganishwa na tarjumi zilizotangulia za Kirussia. Tarjumi yake hiyo ilikamilika mwaka 1991 na kukabidhiwa Akademia ya Kiislamu ya Al Azhar kwa ajili ya kuchunguzwa kabla ya kuchapishwa.

Katika mahojiano mwaka 2011, anasema: "Wakati niliposoma Qur'ani, nilivutiwa sana na nikaamua kuaandika tarjumi yake kwa Kirussia."

Alisema alikumbana na changamoto kadhaa katika kazi yake lakini alipata msaada mkubwa kutoka wanazuoni maarufu hasa Sheikh Ahmad Kaftar, mufti wa zamani wa Syria.

3839564

Name:
Email:
* Comment: