IQNA

11:01 - December 21, 2019
News ID: 3472292
TEHRAN (IQNA) – Wanasayansi Waislamu na wanaharakati wametakiwa kujitokeza wazi katika matukio ya kimataifa kwa lengo la kuutetea Uislamu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Malaysia Saifuddin Abdullah wakati akihitubu katika Mkutano wa Kimataifa Kuala Lumpur 2019 katika jopo la wataalamu waliojadili 'Kulinda Utambulisho wa Kitaifa'.

Ameongeza kuwa, kujitokeza wanasayansi na wanaharakati kutakuwa na taathira chanya ili kuhakikisha kuwa majukwaa kama hayo ya kimataifa hayatawaliwi na watu wanaouchukia Uislamu.

Ametoa mfano na kusema katika masuala kama vile upangaji uzaji na uavyaji wa mimba sauti za Waislamu hazisikiki na kuongeza kuwa, "tunahitaji kujitokeza na kuongoza mijadala kama ile ya demokrasia na haki za binadamu."

Saifuddin amesema kuna udharura mkubwa kwa Waislamu wanaoishi katika nchi zisizo za Kiislamu kuchukua hatua za kulinda utambulisho wao. Kuhusiana na Kanali ya Televisheni iliyopendekezwa ya kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) ambayo itafadhiliwa na Malaysia, Uturuki na Paistan, Saifuddin amesema wako mbioni kufanikisha mradi huo na ametoa wito kwa nchi za Kiislamu kuchangia katika kufanikisha televisheni hiyo.

Kikao cha viongozi wa nchi za Kiislamu cha "Kuala Lumpur 2019" kilianza Alhamisi, na kuhudhuriwa pia na viongozi wengine muhimu wa ulimwengu wa Kiislamu ambao ni mwenyeji, Waziri Mkuu Mahathir Mohammad wa Malaysia, Rais Hassan Rouhani wa Iran, Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani. 

3470152

 

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: