IQNA

11:58 - January 03, 2020
News ID: 3472328
TEHRAN (IQNA) - Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Luteni Jenerali Qassem Suleimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hasdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes wameuawa shahidi mapema leo Ijumaa katika shambulizi la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika barabara ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mapema leo umeshambuliwa kwa maroketi ya helikopta za Marekani. Maafisa wa Marekani wamekiri katika mahojiano yao na shirika la habari la Reuters kwamba, shambulizi hilo limefanyika dhidi ya watu wawili wenye mfungamano na Iran.

Vilevile ndege za zisizo na rubani za Marekani usiku wa Jumapili iliyopita zilishambulia vituo vya harakati ya al Hashdul Shaabi katika mji wa al Qaim kwenye eneo lililoko katika mpaka wa Iraq na Syria na kuua wanachama wasiopungua 25 wa harakati hiyo. Wapiganaji wengine 51 wa al Hashdul Shaabi walijeruhiwa.

Baada ya shambulizi hilo maelfu ya Wairaq walifanya maandamano na mgomo mkubwa mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Baghdad wakipinga shambulizi la Marekani dhidi ya vituo vya harakati hiyo. Makundi na vyama mbalimbali vya siasa vya Iraq pia vimepinga vikali shambulizi la Marekani dhidi ya al Hashdul Shaabi.     

3868478

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: