IQNA

11:13 - January 18, 2020
News ID: 3472382
TEHRAN (IQNA) -Hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa jana mjini Tehran, imeakisiwa sana na vyombo vya habari vya kigeni.

Sambamba na kukaribia tarehe ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Swala ya Ijumaa ya jana mjini Tehran iliongozwa na Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ambapo ilihudhuriwa na mamilioni ya wananchi wa Iran wenye muono wa mbali na wanamapinduzi imara, kwenye eneo la Musalla wa Imam Khomeini (MA) mjini Tehran. Katika uwanja huo Shirika la Habari la Sputnik la Russia limeandika kwamba katika hotuba hiyo ya Swala ya Ijumaa, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alitangaza kuwa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC, ni cha wanamapambano wasio na mpaka. Aidha kanali ya televisheni ya Al-Mayadin ya Lebanon sambamba na kuakisi hotuba ya Ayatullah Sayyid Ali Khamenei imetangaza kwamba, Kiongozi Muadhamu ameitaja siku ambayo Jeshi la IRGC lilishambulia kambi ya jeshi la Marekani nchini Iraq kuwa ni 'Siku ya Mwenyezi Mungu.'

Nalo Shirika la Habari la Reuters limeelezea hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ambayo imezikosoa nchi za Ulaya na kuandika kuwa, kiongozi huyo mkuu wa Iran amezitaja nchi za Ulaya kuwa zisizoaminika kuhusiana na mapatano ya JCPOA. Jarida la Der Spiegel la Ujerumani pia limeelezea hotuba ya Ayatullah Sayyid Ali Khamenei kwamba, kiongozi mkuu wa Iran ametahadharisha kuhusiana na kutoaminika mataifa ya Ulaya kwenye mapatano ya nyuklia ya JCPOA. Aidha mtandao wa habari wa televisheni ya Euronews umeandika kwamba, kiongozi wa Iran amekitaja kitendo cha kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani kuwa ni cha udhaifu uliokita mzizi ndani ya Marekani. Shirika la Habari la Associated Press nalo limeandika kuhusiana na ukosoaji wa Kiongozi Muadhamu juu ya jumbe za Trump ambaye anajifanya kuwatetea raia wa Iran na kuzionya nchi za Ulaya kwa kusema: "Nyinyi ni wadogo sana kuweza kulipigisha magoti taifa la Iran." Aidha mashirika ya habari kama vile ya Bloomberg, Al Jazeera, gazeti la Asharq Al-Awsat kadhalika yameakisi kwa namna tofauti hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu hapo jana Ijumaa.

3872189

Hotuba ya Sala ya Ijumaa ya Kiongozi Muadhamu yaakisiwa na vyombo vya habari duniani

Hotuba ya Sala ya Ijumaa ya Kiongozi Muadhamu yaakisiwa na vyombo vya habari duniani

Hotuba ya Sala ya Ijumaa ya Kiongozi Muadhamu yaakisiwa na vyombo vya habari duniani

Hotuba ya Sala ya Ijumaa ya Kiongozi Muadhamu yaakisiwa na vyombo vya habari duniani

Hotuba ya Sala ya Ijumaa ya Kiongozi Muadhamu yaakisiwa na vyombo vya habari duniani

Hotuba ya Sala ya Ijumaa ya Kiongozi Muadhamu yaakisiwa na vyombo vya habari duniani

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: