IQNA

18:54 - February 08, 2020
News ID: 3472450
TEHRAN (IQNA) - Waislamu wa Slovenia wameshiriki katika Sala ya kwanza ya Ijumaa katika msikiti pekee nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa, sala hiyo iliyodhudhuriwa na mamia ya waumini ilisalishwa na Mufti wa nchi hiyo Sheikh Nedzad Grabus.
Msikiti huo wa kwanza kabisa katika historia ya Slovenia ulifunguliwa Jumatatu katika mji mkuu, Ljubljana baada ya Waisalmu kuvuka vizingiti ya kifedha na upinzani wa watu wenye mismamo mikali ya mrengo wakulia.
Msikiti huo umefunguliwa baada ya kupita miaka 50 tokea litolewa ombi la kutaka eneo hilo la ibada lijengwe. Wapinzani wa mradi huo wamekuwa wakitumia kila mbinu kupinga ujenzi wa msikiti huo ikiwa ni pamoja na kuweka vichwa vya nguruwe katika ardhi ya msikiti huo. Aidha wapinzani wa msikiti huo walipinga vikali hatua ya Qatar kufadhili ujenzi wake wakidai kuwa nchi hiyo inaunga mkono ugaidi.
Mkuu Nedzad Grabu alisema ujenzi wa msikiti huo ni tukio la kihistoria kwa maisha ya Waislamu.
"Slovenia ni nchi ya mwisho ya Yugosalvia ya zamani kupata msikiti," amewaambia waandishi habari.
Waislamu wanakadiriwa kuwa ni asilimi 2.5 kati ya watu wote milioni mbili nchini humo ambapo idadi yao inakadiriwa kuwa ni 80,000.
Slovenia ni nchi ya Ulaya ya Kati, mashariki kwa milima ya Alpi. Imepakana na Italia, Ghuba ya Adria ya Bahari ya Mediteranea, Kroatia, Hungaria na Austria na ni mwanachama wa wa Umoja wa Ulaya.

3877232

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: