IQNA

Msikiti wateketezwa moto India huku maandamano kupinga sheria ya uraia yakiendelea

11:40 - February 26, 2020
Habari ID: 3472507
TEHRAN (IQNA) – Msikiti umeteketezwa moto Jumanne katika mtaa wa Ashok Vihar katika mji mkuu wa India, New Delhi huku maandamano ya kupinga sheria mpya ya uraia yakiendelea.

Kwa mujibu wa taarifa genge la Wahindu wenye misimamo mikali walitekeleza jinai hiyo huku wakiimba nara za  'Jai Shri Ram' na 'Hinduon ka Hindustan" (India ni ya Wahindu).  Aidha genge hilo pia lilipora madoka yote yaliyokuwa karibu na msikiti huo na hakuna maafisa wa polisi waliofika hapo wakati wa jinai hiyo.

Taarifa zinasema watu wasiopungua 10 waliuawa katika eneo hilo la kaskazini mwa New Delhi huku wengine wakijeruhiwa katika maandamano ya Jumatatu alasiri.  Waungaji mkono wa sheria hiyo ya uraia walipambana na wanaopinga sheria hiyo kuanzia Jumapili jioni.

Muswada wa uraia ulio dhidi ya Waislamu na ambao tayari umekuwa sheria, unawapa uraia wahajiri wasio Waislamu waliokimbilia India kutoka nchi jirani za bangladesh, Pakistan na Afghanistan, huku ukiwanyima haki hiyo ya uraia Waislamu.

3470756

captcha