IQNA

Azimio la kwanza la Umoja wa Mataifa kuhusu vita dhidi ya corona

17:45 - April 03, 2020
Habari ID: 3472629
TEHRAN (IQNA) - Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio lake la kwanza kuhusu vita dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 au corona ambapo limetoa wito wa kuweko ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo hatari.

Katika kikao cha jana Alhamisi,  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lilipasisha kwa pamoja azimio linalotaka kuweko ushirikiano wa kimataifa wa kupambana na maradhi ya COVID-19. Hilo ni azimio la kwanza kupasishwa tangu virusi hivyo vilivyopoibuka mwishoni mwa mwaka jana huko Wuhan China.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, azimio hilo linasisitiza kuheshimiwa kukamilifu haki za binadamu na wakati huo huo linapinga vikali ubaguzi wa aina yoyote ile au uenezaji chuki dhidi ya wageni katika fremu ya kukabiliana na virusi vya corona.

Aidha azimio hilo na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linatilia mkazo juu ya nafasi muhimu ya Umoja wa Mataifa katika mgogoro huu wa kiafya na kiuchumi duniani.

Kinyume na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, azimio nambari 193 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa halina ulazima wa kulitekeleza lakini lina thamani ya kisiasa ya kuzingatiwa kwa nchi ambazo zinaliunga mkono.

Licha ya jitihada kubwa, lakini hadi sasa Baraza la Usalama la Usalama la Umoja wa Mataifa linajafikia msimamo wa pamoja kuhusiana na virusi hivi vya corona, huku mivutano ikishuhudiwa kuendelea baina yya nchi mbalimbali hususan baina ya wanachama wawili wa kudumuu wa baraza hilo yaani China na Marekani.

Hadi kufikia sasa watu 1,039,157 wameambukizwa corona kote duniani huku idadi ya waliofariki ikipindukia 55,149. Marekani inaongoza kwa idadi ya walioambukizwa ambao hadi kufikia sasa ni 245,442 huku waliofariki wakiwa ni zaidi ya 6,000. Italia ndio iliyo na watu wengi zaidi walipoteza maisha kutokana na corona duniani ambapo hadi kufikia sasa watu 13,915 wamepoteza maisha katika nchi hiyo ya Ulaya.

3888766

captcha