IQNA

Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajioun

Qarii mashuhuri wa Misri, Sheikh Asfour ameaga dunia

11:52 - April 18, 2020
Habari ID: 3472678
TEHRAN (IQNA) – Qarii (msomaji) mashuhuri wa Qur’ani Tukufu nchini Misri Sheikh Muhammad Mahmoud Asfour ameaga dunia Ijumaa akiwa na umri wa miaka 82.

Kwa mujibu wa taarifa  marhhoum Sheikh Asfour ambaye alikuwa qarii maarufu katika radio nchini humo alizikwa Ijumaa katika mji  waZefta jimboni Gharbia.

Mwendazke alizaliwa mwaka 1938 katika kijiji la Mit al-Rakha, jimbo la Gharbia, kaskazini mwa Misri na alianza kusoma Qur’ani Tukufu akiwa mototo mdogo na alifanikiwa kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 9.

Alijifunza Tajweed na Qiraa ya Qur’ani Tukufu kutoka kwa Sheikh Mustafa Mahmoud al-Anosui. Akiwa nna umri wa miaka 13 alipokea cheti cha Tajweed kutoka kwa Sheikh Anousi.

Alianza kusoma Qur’ani katika misikiti na hafla mbali mbali na baada ya muda usio mrefu umashuhuri wake ulivuma kote Misri.

Harakati za Qur’ani Misri zimeifanya nchi hiyo iwe na wasomaji bora zaidi wa Qur’ani katika ulimwenguni.

3892231

captcha