IQNA

14:34 - January 20, 2020
News ID: 3472388
TEHRAN (IQNA) – Kasisi Mkristo ambaye alikuwa anasikiliza qiraa ya Qur'ani Tukufu nchini Misri alivutiwa sana na usomaji huo na akatoa shukrani zake kwa kumkumbatia.

Kwa mujibu wa taarifa, Rafael Wassil alivutiwa na usomaji wa aina yake wa Qarii Sheikh Taha Al Numani na katika kutoa shurkani alimkumbatia.

Sheikh Al Numani alikuwa anasoma aya za Qur'an katika khitma huko Dikrnis, katika  jimbo la Dakahlia.

Wakristo wa dhehebu la Kikopti ni karibu asilimia 10 ya watu wote Misri, yenye idadi ya watu milioni 100 wengi wakiwa ni Waislamu wa madhehebu ya Sunni. Waislamu na Wakristo nchini Misri wanaishi pamoja kwa amani na hualikana katika mijumuiko ya kidini na kijamii.

Wasomaji maarufu wa Qur'ani Misri ni pamoja na Abdul Basit Abdus Samad, Mohammed Siddiq Al-Minshawi, Shahat Mohamed Anwar, na Mustafa Esmail.

 

 
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: