Kwa mujibu wa Ofisi ya Mawasiliano ya Umma ya Al Kauthar, mashindano ya mwaka huu ambayo yameendelea katika usiku wa nne kwa kuwashirikisha Minhaj Kashif wa Pakistan, Hamed Adel wa Afghanistan, Muslim Abd al-Hussein wa Iraq and Amir Mohammad Khaleghi wa Iran.
Jopo la majaji katika mashindano ya mwaka huu ni wataalamu na wanazuoni wa Qurani Tukufu kutoka Iran, Misri, Syria, Afghanistan na Lebanon.
Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ambayo huandaliwa na Televisheni ya Al Kauthar yamepewa aya ya Qur’ani Tukufu isemayo إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا , "Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu". (Qur’ani Tukufu 78:31).
Mashindano hayo, ambayo yametajwa kuwa kati ya makubwa zaidi ya aina yake duniani, yatakuwa yanarushwa hewani kuanzia saa tano unusu usiku(23:30) kwa wakati wa Tehran au saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki kupitia Televisheni ya Kimataifa ya Al Kauthar na fainali zitafanyika katika siku ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Kwa maelezo zaidi kuhusu mashindano hayo na namna ya kujisajili, bonyeza hapa.