IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu kwa njia ya televisheni

Usajili wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Al-Kawthar TV

18:57 - January 31, 2023
Habari ID: 3476495
TEHRAN (IQNA) - Usajili wa wanaotaka kushiriki toleo la 16 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Kanali ya Televisheni ya Al-Kawthar TV utaanza Jumamosi, Februari 4.

Kwa mujibu wa tovuti ya Al-Kawtahr TV, uzinduzi wa usajili utaambatana na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam Ali (AS).

Tarehe ya mwisho ya kujiandikisha itakuwa Machi 8, sambamba na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam wa Zama, Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake).

Wale walio tayari kushiriki katika mashindano haya ya Qur'ani Tukufu wanaweza kujiandikisha kupitia tovuti ya mafaza.alkawthartv.ir

Walioa na nia ya kushiriki wanatakiwa kutuma faili iliyorekodiwa ya kisomo chao moja ya aya zifuatazo: Aya za 161 hadi 165 za Sura Al-An’am, au aya 142 hadi 144 za Sura Al-A’raf, au aya 110 hadi 115 za Sura Hud.

Muda wa kisomo unapaswa kuwa kati ya dakika mbili hadi tatu.

Faili zilizowasilishwa zijumuishe jina kamili la qari, nchi anayowakilisha na nambari yake ya simu.

Qiraa zitakayowasilishwa zitachambuliwa na jopo la wataalamu wa Qur'ani Tukufu na washindani 96 watachaguliwa kuwania tuzo ya juu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kati yao, 24 watafuzu kwa nusu fainali na hatimaye qaris 5 bora watachuana katika raundi ya mwisho usiku wa kabla ya Eid Al-Fitr.

Mashindano hayo ya Qur'ani Tukufu yanayofanyika kwa njia ya simu yamepewa anuani ya "Inna lil-Muttaqina Mafaza" (Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu- Quran Tukufu, Surat AnNabaa  aya ya 31) hufanyika kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Ni mashindano makubwa zaidi ya ulimwengu ya Kiislamu ya usomaji wa Qur'ani moja kwa moja kwa njia ya televisheni yanayorushwa na Al-Kawthar, Televisheni ya lugha ya Kiarabu ya Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Ili kushiriki katika mashindano haya muhimu ya Qur'ani Tukufu tafadhali bonyeza HAPA

4118576

captcha