IQNA

11:50 - June 22, 2020
News ID: 3472886
TEHRAN (IQNA) – Kamati andalizi ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran haijaafiki pendekezo la mashindano hayo kufanyika kwa njia ya intaneti.

Katika mkutano uliofanyika Jumapili kamati hiyo imetathimini mapendekezo kadhaa kuhusu kufanyika Mashindano ya 37 ya Kimataifa ya Qur'ani ambapo moja ya mapendekezo ni kufanyika mashindano hayo kwa njia ya intaneti lakini pendekezo hilo lilipingwa.

Mashindano ya 37 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalikuwa yamepangwa kufanyika Aprili 10-14 lakini yaliakhirishwa kutokana na wasi wasi wa kuenea COVID-19.

Kamati andalizi imependekeza kuwa mashindano hayo yaakhirishwe kutokana na kuenea janga la COVID-19.

Shirika la Wakfu la Iran huandaa mashindano hayo ya Qur'ani kila mwaka kwa kuwaaliska washiriki kutoka kila kona ya dunia.

Mashindano yam waka jana yalifanyika Tehran na yalikuwa na washiriki kutoka zaidi ya nchi 80 duniani.

3906025

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: