IQNA

19:22 - March 31, 2020
News ID: 3472620
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu nchini Indonesia yameakhirishwa kutokana na hofu ya kuenea ugonjwa wa COVID-19 au corona.

Wizara ya Masuala ya Kiislamu na Daawah nchini Saudia imesema mashindano ya 22 ya kitaifa ya kusoma, kuhifadhi na kufasiri Qur'ani Tukufu ambayo yanajulikana rasmi kama Zawadi ya Mfalme Salman, yameakhirishwa.

Mashindano hayo yalikuwa yafanyika katika mwezi huu wa Shaaban lakini yaliakhirishwa kutokana na hofu ya kuenea corona, imesema taarifa ya wizara.

Tarehe ya mashindano hayo itatangazwa baadaye imesema ripoti hiyo.

Karibu watu 1,300 wameambukizwa corona nchini Saudia Arabia hadi akufikia Jumapili huku wengine nane wakifariki dunia.

3888169

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: