IQNA

Magaidi wa ISIS wakamatwa Libya

20:51 - July 07, 2020
Habari ID: 3472939
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Libya imetangaza kuwakamata magaidi wa kundi la ISIS au Daesh karibu na mji mkuu wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Taarifa ya wizara hiyo imesema magaidi hao wa ISIS wamekamatwa katika mji wa Al-Zawiya yapata kilomita 45 magharibi mwa mji mkuu, Tripoli.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Libya inasema magaidi hao wameingia nchini humo kwa lengo la kuvuruga usalama.

Libya ilitumbukia katika machafuko na vita vya ndani baada ya wanajeshi wa Marekani wakishirikiana na wale wa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) kuishambulia nchi hiyo na kusaidia harakati za kumuondoa madarakani aliyekuwa kiongozi wa nchi Muammar Gaddafi hapo mwaka 2011.

Ni vyema kuashiria kuwa, Libya ina serikali mbili hasimu, moja ikiwa na makao yake mjini Tobruk, iliyoko karibu na Jenerali Haftar, na nyingine ya Serikali ya Mapatano ya Kitaifa Libya inayoongozwa na Waziri Mkuu Fayez al-Sarraj inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa. Haftar anapata uungaji mkono wa kijeshi kutoka Umoja wa Falme za Kiarbau, Misri, Saudi Arabia na baadhi ya nchi za Ulaya.

Machafuko yanayoshuhudiwa Libya yametoa mwanya kwa magaidi wa ISIS kujipenyeza nchini humo.

3909146

Kishikizo: libya ، magaidi ، isis
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha