IQNA

UN: Kuna magaidi 10,000 wa ISIS huko Iraq na Syria, wengine wamefika Afrika

19:02 - August 25, 2020
Habari ID: 3473101
TEHRAN (IQNA) - Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa kuna magaidi zaidi ya 10,000 wa kundi la ISIS au Daesh ambao bado wanaendeleza harakati zao Iraq na Syria ikiwa imepita miaka miwili tokea kundi hilo lishindwe vitani katika nchi hizo.

Mkuu wa Idara ya Kupambana na Ugaidi katika Umoja wa Mataifa Vladimir Voronkov ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa magaidi wa ISIS wanaingia na kutoka Iraq wakiwa katika makundi madogo madogo. Aidha amesema mwaka huu kumeshuhudiwa ongezeko la hujuma za magaidi hao wa ISIS katika nchi hizo jirani.

Voronkov ameongeza kuwa sit u kuwa kundi la ISIS limeaza kujikusnaya tena na kukithirisha vitendo vya kigaidi katika maeneo yasiyo na usalama Iraq na Syria, bali pia matawi ya kundi hilo katika baadhi ya nchi zingine nayo pia yameanzisha harakati.

Ameongeza kuwa hatua zilizochukuliwa na nchi nyingi za kuzuia harakati wakati wa janga la COVID-19 zimepelekea kupungua uwezekano wa hujuma za kigaidi.

Hatahivyo Voronkov amesema kuna ongezeko la mashambulizi ya kigaidi ya watu binafsi ambao wanavutiwa na propaganda za ISIS katika mitandao ya intaneti.

Aidha Voronkov amesema ISIS imeanzisha eneo linalojulikana kama Jimbo la ISIS Afrika Magharibi (ISWAP) ambapo ina wafuasia karibu 3,500. Hivi karibuni ISWAP ilitekeleza mashambulizi kaskazini mwa Nigeria katika jimbo la Borno.

Halikadhalika Mkuu wa Idara ya Kupambana na Ugaidi katika Umoja wa Mataifa amesema kundi hilo linaendeleza mikakati yakie katika eneo la Sahara hasa katika nchi kama vile Burkina Faso, Mali na Niger. Aidha ameashiria kuhusu eneo jingine la ISIS barani Afrika ambalo linajulikana kama  Jimbo la ISIS Afrika ya Kati. Katika eneo hilo magaidi wa ISIS wametekeleza hujuma huko Congo na Msumbuji ambako wamefanikiwa kuteka vijiji kikamilifu.

Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa Vassily Nebenzi amesema hivi sasa kundi la ISIS limebadilisha muundo wake na sasa lina makundi madogo madogo katika nchi mbali mbali duniani.

3472376

captcha