IQNA

23:03 - August 04, 2020
News ID: 3473034
TEHRAN (IQNA) - Mlipuko mkubwa umeutikisa mji mkuu wa Lebanon, Beirut ambapo taarifa zinasema watu wasiopungua 100 wamepoteza maisha. Yamkini idadi hiyo ikaongezeka kwani baadhi ya waliojueruhiwa wako katika hali mahututi.

Taarifa zinasema maelfu ya watu wengine wamejeruhiwa katika mlipuko huo umejiri leo jioni karibu na Bandari ya Beirut.

Shirika Rasmi la Habari la Lebanon limetangaza kuwa mlipuko huo umejiri katika ghala nambari 12 la Bandari ya Beirut na kwamba sababu ya moto ni mada za milipuko ambazo zilkuwa zimehifadhiwa hapo.

Mlipuko huo ulikuwa mkubwa kiasi cha kusikika kilomita nyingi kutoka eneo la tukio.

Taarifa za awali zinasema watu zaidi ya 4,000 wamejeruhiwa na kwamba wanapata matibabu hospitalini.

Kwa mujibu wa taarifa, mlipuko huo umesababisha hasara kubwa kwa nyumba za makazi na pia katika idara binafsi na za serikali. 

 Bado haijafahamika kilichosababisha mripuko huo, hata hivyo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Lebanon, Mohammed Fahmi, amesema huenda shehena kubwa ya kemikali ya ammonium nitrate kwenye bandari ya Beirut iliripuka. 

Waziri Mkuu wa Lebanon Hassan Diab ametangaza Jumatano 5 Agosti itakuwa siku ya maombolezo ya kitaifa kufuatia maafa yaliyosababishwa na mlipuko huo.

Naye Rais Michel Aoun wa Lebanon ameitisha kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Ulinzi wa Kitaifa katika Kasri ya Rais mjini Beirut.

 

3914734

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: