IQNA

19:58 - August 05, 2020
News ID: 3473035
TEHRAN (IQNA) – Rais Hassan Rouhani wa Iran amemtumia ujumbe wa rambi rambi mwenzake wa Lebanon Michel Aoun kufuatia miripuko iliyojiri katika mji mkuu wan chi hiyo Beirut.

Katika ujumbe wake, Rais Rouhani amesema Iran iko tayari kutuma misaada ya dawa, kitiba na misaada mingine inayohitajika katika nchi hiyo.

Wakati huo huo, Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetuma shehena ya kwanza ya misaada ya dharura ya dawa, vifaa vya tiba na chakula nchini Lebanon kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mlipuko wa jana mjini Beirut.

Msemaji wa Hilali Nyekundu ya Iran Mohammad Nasiri amesema kufuatia mlipuko huo wa Beirut, Hilali Nyekundu ya Iran itatuma shehena kadhaa za misaada. Aidha amesema Hilali Nyekundu ya Iran itafungua hospitali ya muda na kutuma timu ya madaktari na wahudumu wa afya 22 Lebanon katika awamu ya kwanza. Amesema misaada hiyo inatumwa kufuatia ombi la mkuu wa Hilali Nyekundu ya Lebanon George Kataneh.

Idadi ya watu waliouawa kwenye mripuko mkubwa katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut, imepindukia 100, huku wengine 4,000 wakiwa wamejeruhiwa. Bado haijafahamika kilichosababisha mripuko huo, hata hivyo Waziri wa Mambo ya Ndani wa Lebanon, Mohammed Fahmi, amesema huenda shehena kubwa ya kemikali ya ammonium nitrate kwenye bandari ya Beirut iliripuka. 

3914801

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: