IQNA

23:09 - August 06, 2020
News ID: 3473040
TEHRAN (IQNA) – Mbunge wa zamani wa utawala haramu wa Israel amebainisha furaha yake kufuatia mlipuko uliojiri katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut kuua idadi kubwa ya watu.

Moshe Feiglin, mbunge wa zamani katika utawala huo haramu na kiongozi wa chama chenye mielekeo ya utaifa ameonyesha kufurahishwa na kutokea mripuko huo wa kutisha ndani ya Lebanon na hata akaandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba, mripuko katika bandari ya Beirut ni "onyesho la kuvutia la fashifashi" lililotokea wakati wa kukaribia moja ya maadhmisho ya Kiyahudi.

Idadi ya watu waliofariki katika mripuko uliotokea Jumanne usiku katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut imefikia 137 na wengine wapato elfu tano wamejeruhiwa, lakini kuna uwezekano idadi hiyo ya vifo na majeruhi ikaongezeka.

Mbali na maafa makubwa ya roho za watu, mripuko wa Beirut umesababisha hasara kubwa pia ya kiuchumi. Meya wa mji mkuu huo wa Lebanon amesema, hasara iliyopata nchi hiyo inakisiwa kufikia mabilioni ya dola. Naye Gavana wa jiji hilo Marwan Abboud amekadiria kuwa, hasara iliyosababishwa na mripuko wa bandari ya Beirut ni kati ya dola ya bilioni 10 hadi 15.

Inaripotiwa kuwa moto uliotokea katika maghala ya mada za milipuko katika bandari hiyo ulisababisha mlipuko mkubwa katika maghala mengine jirani na eneo hilo yaliyokuwa na mada za Ammonium Nitrate.

Lebanon imetangaza siku tatu za maombolezo ya taifa na  jeshi la nchi hiyo limepewa jukumu la kudhamini usalama wa Beirut. Aidha imeamuliwa kuwa, sheria ya hali ya hatari iendelee kutekelezwa mjini Beirut kwa muda wa wiki mbili.   

3472205

Tags: beirut ، mlipuko ، Israel
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: