IQNA

UAE yaisaidia Israel kuanzisha vituo vya ujasusi Yemen

18:38 - August 28, 2020
Habari ID: 3473111
TEHRAN (IQNA)- Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na utawala wa Kizayuni wa Israel zimeafikiana kushirikiana kuanzisha vituo vya ujasusi katika eneo la kistratejia la Socotra huko Yemen.

Ushirikiano huo unakuja kufuatia mapatano yaliyofikiwa kati ya Abu Dhabi na Tel Aviv  ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya pande mbili.

Ujumbe wa pamoja wa wawakilishi wa utawala ghasibu wa Israel na wale wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) wamefunga safari hadi katika eneo la kimkakati la kisiwa cha Socotra nchini Yemen ili kuchunguza maeneo ambayo wataweza kujenga vituo vya kijeshi na ujasusi. 

Lengo la ujenzi wa vituo hivyo limetajwa kuwa ni kufanya ujasusi na kukusanya taarifa kutoka eneo zima la Ghuba ya Uajemi na pia katika Lango Bahari la Babul Mandab na kusini mwa Yemen pamoja na Ghuba ya Aden na eneo la Pembe ya Afrika. 

Kisiwa cha Socotra kipo katika eneo la kistratejia huko katika Lango Bahari la Babul Mandab. UAE imehusika pakubwa katika mauaji ya wananchi wa Yemen kwa kuwa kwake mshirika katika muungano vamizi wa kijeshi dhidi ya Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia. UAE na utawala wa Kizayuni tarehe 13 mwezi huu zilifikia mapatano ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati yao. Mapatano hayo yalifikiwa kufuatia mashinikizo ya Marekani.

3472401

captcha