IQNA

Waliowashambulia wanawake Waislamu Paris wafikishwa mahakamani

11:27 - October 23, 2020
Habari ID: 3473289
TEHRAN (IQNA) – Wanawake wawili ambao waliwashambuliwa wanawake wengine Waislamu waliokuwa wamevaa Hijabu mjini Paris, wamefikishwa kizimbani.

Imearifiwa kwa wanawake hao wawili Wislamu wenye asili ya Algeria walishambuliwa na wanawake wazungu wabaguzi ambao waliwadunga visu na kandokando ya Mnara wa Eiffel  mjini Paris. 
Tukio hilo la wanawake wawili wazungu kuwadunga kisu wanawake hao Waislamu lilijiri Jumapili iliyopita lakini serikali na vyombo vya Ufaransa vilikataa kutoa taarifa yoyote kuhusu hujuma hiyo hadi juzi; suala ambalo limewakasirisha sana watetezi wa haki za binadamu na wadau wa mitandao ya kijamii.

Wanawake hao wawili wa Kiislamu walidungwa visu wakati walipokuwa wakitembelea Mnara wa Eiffel wakiwa pamoja na watoto wao. Hujuma na mashambulizi hayo yaliambatana na matusi yanayowataka Waislamu kuondoka Ufaransa na kurejea katika nchi zao za asili.

Mashambulizi na hujuma dhidi ya Waislamu nchini Ufaransa yameongezeka katika siku chache za hivi karibuni kwa kisingizio cha kupambana na "misimamo mikali".

Ni baada ya raia mmoja aliyetajwa kuwa na "misimamo mikali" kumuua mwalimu wake wa somo la historia.

Ijumaa iliyopita mwanafunzi aliyekuwa na asili ya Chechnia alimuua mwalimu wake baada ya kuwaonyesha wanafunzi darasani picha na vibonzo vinavyomdhalilisha na kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW kwa hoja eti ya uhuru wa kusema. Mwanafunzi huyo pia alipigwa risasi na kuuawa na polisi wa Ufaransa. 

Mwezi Septemba pia Jarida la Kifaransa la Charlie Hebdo , lilichapisha vibonzo vinavyomkebehi na kumvunjia heshima Mtume wa mwisho wa Mwenyezi, Muhammad SAW. Aidha nchini Norway na Sweden wanasiasa wenye misimamo mikali wameshiriki katika vitendo vya kuivunjia heshima Qur’ani Tukufu.

Kuna takribani Waislamu milioni sita Ufaransa wengi wao wakiwa ni wahamiaji kutoka nchi za kaskazini mwa Afrika na idadi hiyo ni takribani asilimia nane ya Wafaransa wote.

3930496

captcha