IQNA

Waislamu Ufaransa

Msichana Mwislamu aishtaki Ufaransa UN kutokana na marufuku ya Hijabu

13:49 - September 23, 2023
Habari ID: 3477639
PARIS (IQNA) - Mwanafunzi wa Kiislamu wa Ufaransa, aliyekataliwa hivi majuzi kuingia shuleni kwake huko Lyon kwa kuvaa vazi la Kijapani la Kimono, amepeleka kesi yake kwenye Umoja wa Mataifa (UN), akisema amebaguliwa kwa misingi ya imani yake ya kidini.

Vazi la Kijapani la Kimono linashabihina kwa kiasi na vazi la Kiislamu la Abaya ambalo limepigwa marufuku Ufaransa.

Tukio hilo ni jingine katika mfululizo wa mizozo inayohusu misimamo ya serikali ya Ufaransa kuhusu vazi la kidini shuleni hususan vazi la hijabu.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 15 kutoka Lyon aliwasilisha malalamiko yake kwa Ashwini K.P., Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu aina za kisasa za ubaguzi wa rangi, ubaguzi, chuki dhidi ya wageni na kutovumiliana. Anasema kuwa kutengwa kwake shuleni mnamo Septemba 5 kulitokana tu na mshikamano wake wa kidini, na hivyo kuashiria tukio jingine la mvutano unaozunguka mavazi ya kidini nchini Ufaransa.

Malalamiko hayo yaliwasilishwa kwa UN kupitia mwakilishi wa kisheria wa msichana huyo, Nabil Boudi, ambaye alitoa taarifa kuhusu suala hilo siku ya Ijumaa. Katika taarifa yake, mlalamishi alikosoa marufuku ya mavazi ya kidini, kama vile hijabu, iliyoanzishwa na Waziri wa Elimu wa Ufaransa Gabriel Attal. Alidai kuwa serikali ya Ufaransa haikuchukua hatua za kutosha kuzuia ubaguzi dhidi ya wanawake.

Hapo awali, mwanafunzi huyo aliwasilisha malalamishi katika Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Lyon, akisema kuwa alibaguliwa kwa misingi ya imani yake ya kidini.

Hata hivyo, mapema mwezi huu, Baraza la Mawaziri la Serikali ya Ufaransa liliunga mkono marufuku ya serikali ya abaya.

Uamuzi huu ulikuja baada ya Vincent Brengarth, wakili anayewakilisha Muslim Rights Action (ADM), kuwasilisha rufaa kwa serikali mnamo Agosti 31, akitaka kusitishwa kwa marufuku hiyo. Brengarth alidai kuwa marufuku hiyo ilikiuka "uhuru kadhaa wa kimsingi."

Serikali ya Ufaransa imekuwa ikikabiliwa na ukosoaji katika miaka ya hivi karibuni kwa sera na matamshi yake yanayolenga jamii za Kiislamu. Haya yamejumuisha uvamizi wa misikiti, uchunguzi katika misingi ya hisani, na kupitishwa kwa sheria ya "kupinga utengano", ambayo inaweka vikwazo vikubwa kwa jamii ya Kiislamu.

Malumbano yanayohusu mavazi ya kidini shuleni yanaendelea kuzua taharuki na mijadala nchini Ufaransa, huku kisa hiki cha hivi majuzi kikiangazia changamoto zinazowakabili wanafunzi wa Kiislamu wanaochagua kueleza imani yao kupitia mavazi yao.

3485274

Habari zinazohusiana
Kishikizo: hijabu ufaransa
captcha