IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Marufuku ya Hijabu katika Michezo ya Olimpiki Yafichua Misimamo mikali ya Kisiasa ya Ufaransa

18:42 - October 07, 2023
Habari ID: 3477696
PARIS (IQNA) - Mwanafikra wa Morocco amekosoa uamuzi wa Ufaransa wa kuwakataza wanariadha wake kuvaa hijabu ambayo huvaliwa na baadhi ya wanawake wa Kiislamu, wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, akisema inafichua upofu na msimamo mkali wa mawazo ya kisiasa ya Ufaransa.

Marufuku ya Hijabu katika Michezo ya Olimpiki Yafichua Misimamo mikali ya Kisiasa ya Ufaransa

PARIS (IQNA) - Mwanafikra wa Morocco amekosoa uamuzi wa Ufaransa wa kuwakataza wanariadha wake kuvaa hijabu ambayo huvaliwa na baadhi ya wanawake wa Kiislamu, wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, akisema inafichua upofu na msimamo mkali wa mawazo ya kisiasa ya Ufaransa.

Mohammad Talabi, mkuu wa Jukwaa la Wasatyea (Msimamo wa wastani) lenye makao yake makuu nchini Morocco, aliliambia Shirika la Anadolu siku ya Ijumaa kwamba marufuku ya hijabu inaonyesha kwamba Ufaransa haiko katika mzozo tu na idadi yake ya Waislamu, bali pia na Afrika nzima na ulimwengu wa Kiislamu.

Alisema uamuzi huo unaonyesha ukosefu wa busara katika fikra za Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye anaongoza misimamo mikali ya dhidi ya dini na uhuru wa Waislamu nchini Ufaransa.

"Maamuzi kama haya yanaonyesha kuwa akili ya kisiasa ya Ufaransa imeambukizwa na itikadi kali, na itaisha na kushindwa vibaya ndani ya Ufaransa na nje," Talabi alisema.

Talabi alisema marufuku ya hijabu itaathiri uaminifu wa watu wa Ufaransa na Waislamu wa Ufaransa kwa jimbo lao, kwani wanashuhudia maandamano na vurugu kote nchini.

Mwishoni mmwa mwezi Septemba Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa imepinga mpango wa Ufaransa wa kupiga marufuku vazi la hijabu katika michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.

Siku chache baada ya hatua tata ya Waziri wa Michezo wa Ufaransa, Amelie Odia-Castera, Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa imetangaza kwamba, hakutakuwa na vikwazo vya hijab kwa wanariadha katika Michezo ya Olimpiki ya Paris, ambayo itafanyika Julai 26 hadi Agosti 11, 2024.

Hapo awali, Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa ilikosoa uamuzi wa serikali ya Ufaransa wa kupiga marufuku vazi la hijab kwa wanariadha wa Ufaransa katika Michezo ya Olimpiki ya 2024 mjini Paris.

Katika taarifa yake, Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, ililaani marufuku ya vazi la hijabu nchini Ufaransa, ikisema kuwa nchi hiyo imekiuka mkataba wa kimataifa wa haki za binadamu kwa kuwazuia wanawake na wasichana kuvaa hijabu shuleni na maeneo ya umma.

Kamati ya Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ilitoa taarifa hiyo baada ya Waziri wa Michezo wa Ufaransa kusema Jumapili iliyopita kwamba, wanariadha wa Ufaransa hawataruhusiwa kuvaa hijabu katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka ujao mjini Paris.

/3485459

Kishikizo: hijabu ufaransa olimpiki
captcha