IQNA

Hifadhi kubwa zaidi ya athari za sanaa za Kiislamu mjini Cairo

23:00 - November 19, 2020
Habari ID: 3473375
TEHRAN (IQNA) – Jumba la Makumbusho la Sanaa za Kiislamu Cairo, Misri ni hifadhi kubwa zaidi ya athari za sanaa za Kiislamu duniani.

Jumba hilo la makumbusho lina athari za sanaa za Kiislamu kutoka maeneo mbali mbali ya bara la Afrika, eneo la Iberia la kusini magharibi mwa Ulaya, Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) India, China na maeneo mengine duniani.

Jumba la Makumbusho la Sanaa za Kiislamu Cairo limeweka katika maonyesho athari 4,500 za sanaa za Kiislamu katika kumbi 25 lakini kwa ujumla  jumba hilo la makumbusho lina hifadhi ya athari zaidi ya 100,000 za sanaa za Kiislamu.

Jumba la Makumbusho la Sanaa za Kiislamu Cairo lilianzishwa mwaka 1880 kufuatia amri ya mtawala wa wakati huo wa Misri Khedive Ismail Pasha na ujenzi wake ulimalizika mwaka 1902.

3935875/

Kishikizo: misri ، waislamu ، sanaa ، kiislamu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha