IQNA

Swala ya Ijumaa kuanza katika zaidi ya misikiti 480 Sharjah

22:05 - November 25, 2020
Habari ID: 3473394
TEHRAN (IQNA) – Misikiti 487 katika eneo la Sharjah nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) itaruhusiwa tena kuwa na swala za Ijumaa kuanzia Disemba 4.

Kwa mujibu wa Idara ya Kukabiliana na Maafa Sharjah, waumini watajulishwa kuhusu kanuni za kufuatia ili kuzuia maambukizi ya COVID-19.

Idara ya Masuala ya Kiislamu Sharjah imesema misikiti katika eneo hilo inatayarishwa kwa ajili ya swala ya Ijumaa. 

Waumini wametakiwa kuzingatia kanuni za kuzuia kuenea COVID-19 ambazo ni pamoja na kila moja kuja msikitini akiwa na zulia au mkeka binafsiwa wa kuswali, kuvaa barakoa ndani ya msikiti na kudumishwa umbali wa mita mbili baina ya kila muumini msikitini.

Hadi sasa watu 161,000 wameambukizwa COVID-19 nchini UAE na miongoni mwao 559 wamefariki dunia.

3473225/

Kishikizo: msikiti ، swala ya ijumaa ، covid-19 ، UAE
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha