IQNA

Watoto wa Somalia wakisoma Qur’ani katika mazingira magumu + Video

20:28 - December 30, 2020
Habari ID: 3473506
TEHRAN (IQNA) – Madrassah za Qur’ani nchini Somalia maarufu kama Duksi zinaendelea kuwa tumaini kwa watoto nchini humo pamoja na kuwepo mazingira magumu ya kiuchumi, kijamii na umasikini mkubwa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, pamoja na kuwepo hali ngumu ya maisha na kiafya nchini Somalia, ambayo ni kati ya nchi masikini zaidi duniani, lakini Waislamu nchini humo wanahakikisha kuwa watoto wao wanasoma na kuhifadhi Qur’ani Tukufu.

Katika madrassah hizo watoto huandika aya za Qur’ani katika ubao na kisha kuhifadhi aya walizoandika. Mbinu hii ya kuhifadhi Qur’ani imeweza kutumika kwa mafanikio katika nchi zingine za Pembe ya Afrika kama vile Kenya, Ethiopia na Djibouti. Madrassah hizo huwakubali watoto kuanzia miaka mitano na huendelea kuhifadhi Qur’ani hapo hadi wanapofika umri wa miaka 18. Hivi sasa Somalia ni kati ya nchi ambazo zina idadi kubwa ya watoto waliohifadhi Qur’ani Tukufu katika eneo zima la Pembe ya Afrika na mashariki mwa Afrika.

Hivi sasa kutokana na ukosefu wa serikali kuu nchini Somalia nchi hiyo inakumbwa na matatizo makubwa ya usalama na utoaji huduma kwa wananchi ni dhaifu mno. Idadi ya watu Somalia ni takribani milioni 16 na asilimia 99 ya wakazi wa nchi hiyo ni Waislamu.

3944456

captcha