IQNA

Qiraa ya Qur’ani ya Mohammad Badr Hussein katika msikiti mjini Cairo + Video

20:12 - January 05, 2021
Habari ID: 3473525
TEHRAN (IQNA)- Mohammad Badr Hussein, aliyezaliwa mwaka 1937 nchini Misri, alikuwa miongoni mwa wasomaji bora zaidi wa Qur’ani katika zama zake.

Alizaliwa katika familia ya wasomaji na waliohifadhi Qur’ani mwaka 1937 ktika jimbo la Gharbia.

Alianza kusoma Qur’ani akiwa na umri mdogo na akafanikiwa kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu akiwa bado motto. Aliendelea na masomo yake katika Chuo Kikuu cha Al Azhar na akahitimu mwaka 1968.

Mohammad alijiunga na Radio ya Qur’ani nchini Misri mwaka 1961 na kisha akwa qarii rasmi katika televisheni ya taifa mwaka 1963.

Mwaka 1970 alishiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Malaysia na akashifa nafasi ya kwanza katika vitengo vya qiraa na kuhifadhi Qur’ani Tukufu.

Aidha alihudhuria mashindano mengi ya kimataifa ya Qur’ani akiwa miongoni mwa wanaoshindana na kisha kama jaji. Qarii huyu mtajika wa Misri aliaga dunia na kurejea kwa Mola wake Machi 28 mwaka 2002.

Ifuatayo hapa chini ni qiraa yake ya Sura Al-Qiyama katika msikiti mmoja mkongwe mjini Cairo.

captcha