IQNA

Wageni katika 'Maoneysho ya Vitabu Cairo' wapata zawadi ya Qur'ani

19:16 - July 05, 2021
Habari ID: 3474072
TEHRAN (IQNA)- Chuo Kikuu cha Al Azhar kimewatunuku Qur'ani Tukufu wageni katika Maonyesho ya 52 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Cairo, Misri.

Kwa mujibu wa tovuti la Al Ahram wageni hao ambao walikuwa ni wanafunzi walitembezwa katika maonyesho hayo na Muhammad al Mahrasawi, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al Azhar. Wanafunzi hao walijifunza kuhusu sekta ya uchapishaji ya Chuo Kikuu cha Al Azhar pamoja na vitabu vya Kiislamu katika maoneysho hayo. Aidha walishiriki katika warsha iliyoandaliwa katika kibanda cha Al Azhar katika maonyesho hayo.

Mkuu wa Al Azhar aliwatunuku wanafunzi hao ni nakala za Qur'ani Tukufu au misahafu na pia aliwapa barakoa na vitakasa mikono vya kukabiliana na virusi vya corona.

Maoneysho ya 52 ya Vitabu ya Cairo yalianza Juni 30 na yataendelea hadi Julai 15.

3981720

captcha