IQNA

Harakati za Qur'ani Tukufu

Wamisri wamuaga hafidh mkongwe zaidi wa Qur'ani huko Gharbia

16:57 - November 30, 2022
Habari ID: 3476174
TEHRAN (IQNA) - Mamia ya watu walihudhuria mazishi ya Sheikh Mohamed Mahmoud al-Qadim, mwalimu na hafidh wa Qur'ani mzee zaidi katika Mkoa wa Gharbia nchini Misri

Watu kutoka kijiji alikozaliwa cha Kifr al-Mahrouq na vijiji na miji ya karibu pia walishiriki katika mazishi hayo, yaliyofanyika Jumanne baada ya sala ya adhuhuri.

Kulingana na wanakijiji, alikuwa Hafidh wa Qur'ani mwenye umri wa juu  katika jimbo hilo. Watu wengi wa kijiji hicho na wale kutoka sehemu nyingine za mkoa walijifunza na kuhifadhi Qur'ani chini yake.

Quran Tukufu ndiyo maandiko pekee ya kidini ambayo yanahifadhiwa kikamilifu na wafuasi wake ambapo waliohifadhi huweza kusoma aya zote bila kutizama maandishi.

Egyptians Bid Farewell to Oldest Quran Memorizer in Gharbia

Watu wasiohesabika katika kila umma wa Kiislamu wamehifadhi Quran tangu siku ya kwanza ilipoteremshwa.

Qur'ani Tukufu ina Juzuu (sehemu) 30, Sura 114 (sura) na aya 6,236.

4103529

Kishikizo: qurani tukufu ، misri ، gharbia ، al qadim
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha