IQNA

13:25 - March 05, 2021
News ID: 3473705
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya Qur’ani kwa ajili ya wanafunzi wa shule yatafanyika nchini Uganda katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.

Kwa mujibu wa Shirika la Iran la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO), mashindano hayo yatafanyika kwa ushiriano baina ya Radio Bilal FM ya Uganda na Kituo cha Utamaduni cha Iran katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Hivi karibuni Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Uganda Mohammad Reza Qezelsofla  alifanya mazungumzo na mkurugenzi wa Bilal FM Muzaffar Mungumia kuhusu mashindano hayo ya Qur’ani.

آماده//برگزاری مسابقات قرآن رمضانیه در اوگاندا

Inatazamiwa kuwa mashindano hayo yatawajumuisha wanafunzi wa shule za Kiislamu za msingi na upili nchini Uganda. Mashindano hayo yatakuwa katikakategoria za kusoma na kuhifadhi Qur’ani Tukufu.

Kwa mara kadhaa sasa Bilal FM imeshirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Iran katika kuandaa hafla na mijimuiko ya Kiislamu.

3957323   

 

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: