IQNA

Mashindano

Mashindano ya Qur'ani yafanyika kwa wanafunzi nchini Uganda

21:25 - November 04, 2024
Habari ID: 3479698
IQNA - Mashindano ya Qur'ani Tukufu yalifanyika kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa huko Kyengera, mji mkuu wa Uganda wa Kampala, wikendi hii.

Mashindano ya Qur'ani  yafanyika kwa wanafunzi nchini UgandaHafla hiyo ya Qur'ani imeandaliwa na Kituo cha Utamaduni cha Iran katika nchi hiyo ya Kiafrika.
Washindani hao walishindana katika kategoria mbalimbali, zikiwemo za usomaji na kuhifadhi Qur'ani.
Akihutubia sherehe za kufunga, Balozi wa Iran nchini Uganda Majid Saffar amewataka Waislamu kuifanya Qur'ani Tukufu kuwa mwongozo wao mkuu.
Kitabu kitakatifu kina hekima yote ya maisha, alisema, na kuongeza, "Kamwe usigeuke kutoka kwayo."
Pia alisisitiza umoja baina ya Waislamu, akitolea mfano msisitizo wa Qur'ani juu ya uadilifu wa kijamii na kuwalinda wanyonge na wanaodhulumiwa, hususan katika maeneo kama Ukanda wa Gaza, Palestina na Lebanon.
Balozi Saffar aliwakumbusha washiriki kwamba Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) aliwatetea waliodhulumiwa.
Aidha amewahimiza Waislamu kuleta ujumbe wa amani na umoja akisisitiza kuwa wao ni jumuiya moja.
Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Uganda, Bw. Abbasi pia alihutubia sherehe za kufunga na kuwataka Waislamu kuifanya Qur'ani Tukufu kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku.
Amesema kusoma Qur'ani kila siku kunawanufaisha Waislamu duniani na akhera.
Mzungumzaji mwingine alikuwa Sheikh Muhammad Ali Waiswa, naibu wa kwanza wa Mufti, ambaye alitoa wito wa dua maalumu kwa ajili ya Palestina, Lebanon na Syria.
Pia amesema mabeberu wanaendelea kufuata ukoloni mamboleo na unyonyaji.

3490530

Kishikizo: qurani tukufu uganda
captcha