IQNA

Warsha ya Qur'ani Tukufu na Ramadhani yafanyika nchini Uganda

16:48 - April 09, 2022
Habari ID: 3475103
TEHRAN (IQNA)-Warsha imefanyika nchini Uganda kuhusu kuifahamu Qur'ani Tukufu na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Warsha hiyo imeandaliwa kwa ajili ya wanafunzi na wahadhiri katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Metropolitan katika mji mkuu wa Uganda, Kampala.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, warsha hiyo imeandaliwa na Kituo cha Utamaduni cha Iran mjini Kampala na mhadhiri wa warshi hiyo alikuwa ni Mwambata wa Utamaduni wa Iran mjini Kampala Mohammad Reza Qezelsofla.

Kati ya mada muhimu katika mada hiyo zilikuwa ni malengo ya saumu ya Mwezi wa Ramadhani, basira au muono wa mbali na kuwahurumia wanaodhulumiwa.

Pembizoni mwa warsha hiyo kumefanyika mashindano ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu na pia darsa kuhusu mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu.

1401012010432

captcha