IQNA

Iran yakosoa azimio dhidi yake katika Baraza la Haki za Binadamu la UN

19:40 - March 25, 2021
Habari ID: 3473759
TEHRAN (IQNA) - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu azimio dhidi ya Iran lililotolewa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na kusisitiza kuwa, nchi zinazokanyaga haki za mataifa ya dunia hazina ustahiki wa kuzungumzia haki za binadamu.

Saeid Khatibzadeh amesema hayo leo (Jumatano) wakati akijibu azimio lililotolewa na kundi moja la nchi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kikao cha 46 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa, azimio hilo limekosa kura zinazotakiwa, ni dhaifu na halikukubaliwa kimataifa.

Amesema, azimio hilo ni la muendelezo wa ripoti tu za ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa ambaye katika ripoti zake za huko nyuma alishindwa hata kugusia mauaji ya makumi ya watoto wasio na ulinzi na sauti za kuomba misaada za mamia ya wagonjwa wasio na hatia ambao wanashindwa kupata madawa na vifaa vya matibabu. Ripoti zake zimeshindwa angalau kugusia uvunjaji mkubwa wa haki ya kuishi na haki ya kupata matibabu maelfu ya wananchi wa Iran kutokana na vikwazo vya kidhulma vilivyowekwa na maadui.


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia amesema, waliounga mkono azimio hilo, yaani Marekani na watenda jinai wenzake, ndio wanaolifanyia taifa la Iran ugaidi mkubwa wa kiuchumi na vikwazo vya kiwango cha juu na vya kidhalimu ambavyo vimepiga marufuku hata kufika madawa nchini Iran tena wakati wa janga la dunia nzima la ugonjwa hatari wa COVID-19.

Amesema, pamoja na dhulma yote hiyo inayofanyiwa, lakini muda wote Iran imetekeleza vizuri majukumu yake ya kulinda haki za wananchi wake na za jamii ya kimataifa.

3961078

Kishikizo: iran haki za binadamu
captcha