IQNA

Mkutano wa Kimataifa Kujadili Haki za Binadamu kwa Mtazamo wa "Mashariki"

18:31 - April 14, 2025
Habari ID: 3480539
IQNA – Mkutano wa Kimataifa kuhusu "Haki za Binadamu kwa Mtazamo wa Mashariki" unatarajiwa kufanyika tarehe 27 Aprili, 2025, jijini Tehran, na utaendelea tarehe 28 na 29 Aprili katika Chuo Kikuu cha Baqir al-Olum mjini Qom.

Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jumapili, tarehe 13 Aprili, Seyed Hadi Sajjadi, Naibu wa Masuala ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Baqir al-Olum, alieleza malengo na muundo wa tukio hilo.

“Mkutano huu unalenga kuwasilisha mjadala wa kina kuhusu masimulizi ya haki za binadamu yanayotawaliwa na Magharibi,” alisema. “Zaidi ya hayo, tunaunda mfumo mpya unaojumuisha mitazamo ya ustaarabu na dini ambazo kihistoria zimepuuzwa au kutengwa katika kuunda kanuni za kimataifa za haki za binadamu.”

Sajjadi alifafanua kwamba neno "Mashariki" linahusu utamaduni, si kijiografia na linajumuisha mataifa ambayo haki za zimekandamizwa na Wamagharibi.

3492673

Habari zinazohusiana
captcha