Ayatollah Nasser Makarem Shirazi, kiongozi mkuu Kiislamu au Marja Taqlid katika mji wa Qom, alitoa kauli hiyo katika ujumbe wa kufungua mkutano wa 10 wa Haki za Binadamu za Kimarekani Kwa Mtazamo wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
“Kwa miaka mingi, dhana ya juu ya haki za binadamu imekuwa ikitumiwa vibaya na mamlaka za ukandamizaji na wahalifu kutekeleza maslahi yao haramu,” alisema, na kuongeza kuwa, “chini ya mwavuli wa eti kutetea haki za binadamu, wamefanya baadhi ya ukatili mkubwa dhidi ya mataifa na jamii, yote bila kuzingatia dhamiri ya binadamu au kuheshimu haki za mtu binafsi; hali ya sasa katika eneo letu ni ushahidi wazi kabisa wa madai haya.”
“Dunia nzima inashuhudia ukatili unofanywa na utawala wa Israel huko Gaza. Maelfu ya wanawake, watoto, na raia wasio na hatia waliuawa au kukimbia makazi yao kutokana na uhalifu huu ,uhalifu uliotekelezwa na serikali inayotokana na fikra za kikoloni na dhidi ya utu wa binadamu zilizozaliwa Magharibi,” aliongeza.
Ayatullah Makarem Shirazi alikosoa vikali mashambulio ya kikatili ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran mwezi huu ambayo yameua zaidi ya Wairani 900, wakiwemo wanawake na watoto.
“Hatuwezi pia kupuuza mashambulizi ya hivi karibuni ya kigaidi dhidi ya nchi yetu ya Kiislamu, ambapo watu wasio na hatia waliuawa katika mashambulizi ya hovyo dhidi ya makazi yao,” alisema, akijiuliza, “Je, hawa waliopoteza maisha hawakuwa na haki za msingi kama vile maisha na usalama? Walikuwepo katika uwanja wa vita?”
“Ni lazima tuseme wazi: mtazamo wa Magharibi kuhusu ubinadamu na haki za binadamu ni wa kibinafsi,” alisisitiza.
“Mradi tu nguvu na udhibiti wao siyo hatarini, wanazungumza kwa maneno ya heshima. Lakini wakati maslahi yao yanapokuwa hatarini, mhanga wa kwanza huwa ni ‘haki za binadamu’ yenyewe,” aliongeza.
“Hatupaswi kamwe kudanganywa na kauli za uzito za Magharibi. Haki za binadamu wanazotangaza kutetea hazina msingi wala maana. Hawaamini heshima ya binadamu wala hawazingatii kanuni wanazodai kuziunga mkono,” alibainisha.
Aliwataka wasomi na wafuasi wa fani hii kueneza elimu na kufunua ukweli , kuonyesha uso halisi wa wale wanahadaa kuwa eti wanatetea haki za binadamu, akibainisha kuwa dhana hii tukufu haipaswi kuruhusiwa “kubadilishwa au kuharibiwa.”