IQNA

Jinai za Israel

Shajareh: Mauaji ya kimbari ya Gaza yafichua madai bandia ya Magharibi kuhusu haki za binadamu

21:45 - December 10, 2023
Habari ID: 3478015
IQNA- Mwanaharakati wa haki za binadamu mwenye makao yake mjini London, Uingereza anasema jibu la nchi za Magharibi kwa mauaji ya kimbari yanayoendelea kutekelezwa na utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza kwa mara nyingine tena limefichua "uongo" wao kuhusu kujali haki za binadamu.

Desemba 10 imeadhimishwa dunaini kote kama Siku ya Haki za Kibinadamu huku mauaji ya kimbari vya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza yakiwa yanaendelea kwa  miezi miwili na kusababisha vifo vya Wapalestina wasipungua  17,700 wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Wanaharakati wa haki za binadamu kutoka kote ulimwenguni tayari wamefanya maandamano kuwashinikiza viongozi wao wa kisiasa kujitenga na Israeli na kuunga mkono Wapalestina.

Katika mahojiano malaumu na IQNA, Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Kibinadamu ya Kiislamu yenye makao yake London (IHRC) Massoud Shajareh amekosoa  vyombo vya kimataifa kama Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiisalmu, Jumuiya ya Kiarabu, na Mahakama ya Kimataifa kwa kutochukua hatua zozote za maana kukabiliana na mauaji ya kimbari yanayoendelea kutekelezwa na Israel huko Gaza.

Akielezea matukio ya Gaza kama "mauaji ya kikatili zaidi katika maisha yetu yanayotokea mbele ya macho yetu." Mwanaharakati huyo alisema kwamba Wapalestina "wanalengwa kwa makusudi."

Amekosoa vikali  utepetevu wa vyombo vya kimataifa na nchi zinazozungumza tu kuhusu haki za binadamu, akibainisha kuwa badala ya kukimbilia kuwasaidia Wapalestina "zinatuma silaha ... ili kuuwezesha utawala ghasibu wa Kizayunikuua watu zaidi.

Amesema ulimwengu unakabiliwa na "tanziko la kutisha" kwani kuna maswali kuhusu ikiwa Umoja wa Mataifa na taasisi zingine "zimekufa", au kwamba "ubinadamu uko gizani au unatiliwa shaka."

Shajareh alibainisha kuwa licha ya mashinikizo yote kutoka kwa viongozi wa kisiasa, iwe Marekani au kwingineko, kuwanyamazisha watu wanaotetea Palestina, "raia wa kawaida wamefichua udikteta ulioko katika nchi za Magharibi.

Amesema watu wa kawaida kote ulimwenguni wamezinduka na wamegundua kuwa njia ya kukabiliana na utawala wa Israel ni kuanzisha kampeni ya kuususia utawala huo na kuwashinikiza viongozio wa kisiasa wa nchi zao.

/3486357

Habari zinazohusiana
Kishikizo: gaza haki za binadamu
captcha