IQNA

21:46 - March 29, 2021
News ID: 3473769
TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Msumbiji Omar Saranga amewaambia waandishi habari huko Maputo kwamba, jeshi linapambana vikali na waasi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Palma ulioko karibu na mpaka wa nchi hiyo na nchi jirani ya Tanzania.

Magaidi wauteka mji wa Palma Msumbuji, oparesheni ya kuwatimua yaanzaMji huo ambao una akiba kubwa ya gesi inayokadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni 20, ulidhibitiwa na waasi wa al Shabab katika uvamizi uliosababisha mauaji ya makumi ya raia wasio na hatia. 

Saranga amesema jeshi la taifa la Msumbiji linafanya jitihada za kukomesha mashambulizi ya kigaidi ya kundi hilo na kurejesha amani huko Palma na kwamba, oparesheni hiyo ya jeshi imefanikiwa kuokoa maisha ya mamia ya watu wakiwemo raia wa kigeni. 

Wakati huo huo shirika la habari la Reuters limenukuu vyombo vya kidiplomasia na kiusalama kwamba, jeshi la Msumbiji halijafanikiwa bado kukomboa mji wa Palma uliodhibitiwa na waasi Ijumaa iliyopita baada ya mapigano yaliyoendelea kwa masaa 48.

Mji wa Palma uko karibu maili sita kutoka mradi mkubwa wa gesi asili katika eneo la Afungi katika Bahari ya Hindi karibu na mpaka wa Msumbuji na Tanzania.

Habari zinasema maelfu ya raia wa mji huo wameendelea kuyakimbia makazi yao na kutafuta usalama wa roho zao mahala kwingine. 

Watu waliotoroka mji wa Palma wanasema mji huo umeharibiwa kabisa na kuna watu waengi waliouawa katika hujuma ya magaidi.

Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na shambulizi hilo lakini katika miezi ya hivi karibuni kundi la kigaidi linalojiita ISIS Mkoa wa Afrika ya Kati, ambalo linafungamana na kundi la kimataifa la kigaidi la ISIS au Daesh, limehusika na mashambulizi mengi.

3961692

Tags: waislamu ، palma ، msumbuji
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: