IQNA

Chanjo ya Corona ya Sputnik V ni Halali, imetengenezwa kwa kuwazingatia Waislamu

20:21 - February 12, 2021
Habari ID: 3473643
TEHRAN (IQNA) – Vladimir Gushchin mtafiti katika Kituo cha Utafiti wa Gamaleya nchini Russia ambayo imetengenza chanjo ya Corona ya Sputnik V amesema chanjo hiyo ni halali kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.

Daktari Gushchin amesisitiza kuwa hakuna mada yoyote ya wanyama katika chanjo ya Sputnik V.

Ameongeza kuwa wakati walipoanza kutegeneza chanjo ya Corona walizingatia mafundisho ya Kiislamu na hivyo walijizuia kutumia mada zozote za wanyama ambao hawajachinjwa kwa njia halali, nyama ya nguruwe, damu n.k.

Aidha amesema chanjo ya Corona ya Sputnik V imetengenezwa kwa kuzingatia maagizo ya dini ya Kiislamu ambayo yametolewa na Idara ya Masuala ya Waislamu Russia.

Hivi sasa nchi kadhaa za Kiislamu zimeagiza chanjo ya Corona ya Sputnik V. Nchi hizo ni pamoja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Tunisia, Algeria, Pakistan, Lebanon, Bahrain,  na Umoja wa Falme za Kiarabu.

3953529

captcha