IQNA

19:37 - May 02, 2021
Habari ID: 3473869
TEHRAN (IQNA) Maoneysho ya kwanza ya Qur’ani kufanyika kwa njia ya intaneti katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yamefunguliwa Jumamosi.

Ufunguzi wa maonyesho hayo umehudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa Iran akiwemo Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Sayyed Abbas Salehi na Naibu Waziri  anayeshughulikia masuala ya Qur’ani na Etrat Abdul Hadi Faqihzadeh.

Maoneysho hayo Intaneti yatafanyika kwa muda wa siku kumi kupitia tovuti ya https://www.iqfa.ir/

Maoneysho hayo yanajumuisha wachapishaji 500 ambao wanaonyesha vitabu vyo kuhusu maudhui za Qur’ani Tukufu.

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani mwaka jana yalifutwa kutokana na janga la COVID-19 au coroa lakini sasa yanafanyika kwa njia ya itaneti.

Mauzo katika maonyesho hayo ya Qur'ani yatafanyika kwa njia ya itaneti ambapo mashirika yanayouza bidhaa yanalazimika kupunguza bei kwa asilimia 20.

Maoneysho hayo huandaliwa kila mwaka na Wizara ya Utamaduni na Muongozi wa Kiislamu nchini Iran.

Imeamuliwa kuwa hata baada ya kumalizika janga la corona, maonyesho hayo yatakuwa yakifanyika kwa njia ya intaneti na pia katika ukumbi siku za usoni.

Kutokana na janga la corona, shughuli nyingi duniani sasa zinafanyika kwa njia ya intaneti jambo ambalo limepelekea ongezeko kubwa la mauzo ya bidhaa kwa njia hiyo.

3968481

Kishikizo: maonyesho ya qurani ، intaneti ، iran
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: