Tukio hili la kielimu linaandaliwa kwa heshima ya kumbukumbu ya miaka 1,500 tangu kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW), na litawakutanisha wasomi wa vyuo vikuu na taasisi za Kiislamu kutoka mataifa mbalimbali.
Mada zitakazojadiliwa ni pamoja na “Ujumbe wa Kimataifa wa Mtume wa Uislamu (SAW) kwa mujibu wa Qur'an na Hadithi,” “Uvumilivu, Upole na Wastani katika Maisha ya Mtume,” “Mtume Mtukufu (SAW); Kielelezo Bora kwa Vizazi Vyote,” “Maisha ya Mtume (SAW) na Utambuzi wa Utambulisho wa Kidini,” na “Uhai wa Uislamu na Umma Ulio Ungana Dhidi ya Wazo la Utandawazi wa Kimagharibi.”
Hujjatul Islam Seyed Hossein Khademian Noushabadi atatoa hotuba akiwa katika studio ya Mobin ya Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), mjini Tehran, huku wazungumzaji wengine wakishiriki kwa njia ya video. Miongoni mwao ni Ayatullah Sheikh Muhammad Yaqubi kutoka Najaf, Iraq; Profesa Juan Cole wa Chuo Kikuu cha Chicago; Hujjatul Islam Yahya Jahangiri; Dr. Salama Abd Al-Qawi kutoka Al-Azhar; na Sheikh Ghazi Hanina, kiongozi wa Jumuiya ya Wasomi wa Kiislamu wa Lebanon.
Mjadala utaanza saa saba adhuhuri kwa saa za Tehran (sawa na saa tatu na nusu asubuhi GMT na utapeperushwa moja kwa moja kupitia tovuti ya Aparat. Baada ya tukio, hotuba zote zitapatikana kwenye tovuti ya IQNA zikiwa na tafsiri ya Kiajemi au Kifursi.
Tukio hili linatoa fursa adhimu kwa Umma wa Kiislamu kutafakari kwa kina juu ya athari za maisha ya Mtume (SAW) katika kujenga jamii yenye huruma, mshikamano, na utambulisho wa kidini unaostahimili changamoto za kisasa.
3494500