IQNA

13:54 - July 09, 2021
Habari ID: 3474083
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametuma salamu za rambirambi kwa taifa la Palestina kutokana na kufariki dunia Katibu Mkuu wa Kamandi Kuu ya Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Palestina (PFLP—GC), Ahmad Jibril.

Katika ujumbe wake Ayatullah Khamenei amelipa mkono wa pole taifa la Palestina na wapigaji wote wa Jihadi kutokana na kifo cha mwanamapambano huyo shujaa na maarufu Palestina. 

Sehemu moja ya salamu za rambirambi za Ayatullah Khamenei inasema: Ninatoa mkono wa pole kutokana na kifo cha mpiganaji ambaye hakuchoka, Bwana Ahmad Jibril, kwa watu wa Palestina, Mujahidina wote na wanaharakati katika uwanja wa mapambano ya Wapalestina, wana muqawama wote katika eneo la Asia Magharibi na kwa familia yake.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Bwana huyu shujaa na aliyekuwa na bidii alitumia maisha yake kupigania nchi yake iliyoghusubiwa. Vilevile amemuombea maghufira na msamaha  wa Mwenyezi Mungu marehemu Ahmad Jibril.

Mwanamapambano huyo shujaa wa Palestina aliaga dunia Jumatano iliyopita akiwa na umri wa miaka 83 wakati akipata matibabu katika hospitali moja mjini Damascus, Syria. Alikuwa miongoni mwa walioamini kuwa mapambano ya silaha ndio njia pekee ya kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel na kuikomboa Palestina.

Marhum Ahmad Jibril aliwahi kutembelea Iran mara kadhaa na kukutana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kama inavyoonyesha pia iliyo katika habari hii.

3982807

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: