IQNA

Comoro yapokea misaada ya Misahafu kutoka Kuwait

21:41 - August 02, 2021
Habari ID: 3474150
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Kuhuisha Turathi za Kiislamu ya Kuwait imesambaza mamia ya Misahafu na vitabu vya Kiislamu nchini Comoro.

Kwa mujibu wa taarifa vitabu hivyo vya Kiislamu vinasambazwa na jumuiya hiyo kwa lengo la kukabiliana na kile ambacho kinatajwa kuwa kukabiliana na  nisimamo mikali na ya kigaidi nchini Comoro.  Misaada hiyo ya itasambazwa miongoni mwa Makadhi, wanafunzi na maafisa wa serikali ya Comoro.

Sherehe ya kupokea vitabu hivyo vya Kiislamu na Misahafu imefanyika katika Kitivo cha Imam Shafii cha Chuo Kikuu cha Comoro.

Miongoni mwa walioshiriki katika sherehe hiyo ni Waziri wa Masuala ya Kiislamu Comoro Muhammad Hussein Jamalulayl na Sheikh Abdulkarim Mohammad Shakir mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislamu Comoro.

3988021

Kishikizo: comoro ، kuwait ، misahafu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha