IQNA

Mbunge Muislamu Zambia atimuliwa bungeni kwa kuvaa kanzu

11:57 - December 18, 2021
Habari ID: 3474690
TEHRAN (IQNA) – Wasimamizi wa Bunge la Zambia wamemtimua mbunge mmoja Muislamu kwa sababu alikuwa amevaa vazi la kanzu ambalo hunasibishwa na Waislamu.

Mbunge wa Lumezi Munir Zulu ametimuliwa kutoka Bunge la Zambia kwa sababu ya kuvaa kanzu ambalo imedaiwa linakiuka kanuni ya mavazi ya wabunge nchini humo.

Kanzu ni vazi rasmi katika nchi nyingi na huvaliwa na wanaume wakiwa katika kazi zao za kawaida.

Zulu amesisitiza kuwa hajakiuka kanuni za mavazi bungeni na amesema kanuni nambari 206 imetaja kanzi kama miongoni mwa mavazi ya kiutamaduni ya Afrika

Hatahivyo naibu Spika Attractor Malungo amemtimua Lumezi kwa kudai kuwa kanzu haikubaliki kisheria.

3476970

Kishikizo: zambia munir zulu kanzu
captcha