IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya mabarobaro nchini Zambia

11:17 - May 05, 2022
Habari ID: 3475207
TEHRAN (IQNA)- Fainali ya Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya mabarobaro imemalizija Jumatatu wiki hii nchini Zambia.

Mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'ani yameandaliwa na Kituo cha Kiislamu Zambia ambapo vijana walio chini ya umri wa miaka 18 wameshiriki.

Fainali ya mashindano hayo ya Qur'ani imefanyika katika usiku wa mwisho wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Zambia ni nchi iliyo kusini mwa Afrika na ina idadi ya watu karibu milioni 18 ambapo idadi ya Waislamu ni takribani asilimia moja huku Ukristo ukiwa dini rasmi ya nchi.

4054755

captcha